Taiwan yasema China iliteka raia wake

Image caption Taiwan inailaumu China kwa kuwateka raia wake

Taiwan imelaumu polisi nchini Kenya kwa kutumia vitoa machozi na bunduki kuwalazimisha watu 37 kati ya raia wake kuingua ndani ya ndege na kusafirishwa hadi China.

Hili ndilo kundi la pili la raia wa Taiwan kusafirishwa kwenda China ndani ya siku tano.

Baadhi yao walikuwa wameondolewa mashtaka ya ulaghai. Taiwan inailaumu China kwa kuwateka raia wake na kusema kuwa China iliishinikiza Kenya kuingilia kati mzozo huo wa kidiplomasia.

Image caption China inaitaja Taiwan ambayo imejitawala tangu mwaka 1950 kuwa mkoa wake

Kenya haitambui uhuru wa Taiwan na imesema kuwa inafuata sheria ya kuwasafirisha watu kwenda nchini mwao.

China inaitaja Taiwan ambayo imejitawala tangu mwaka 1950 kuwa mkoa wake uliojitenga ambao ni lazima uunganishwe naye.