Waziri wa Italia akutana na serikali ya Tripoli

Haki miliki ya picha EBA
Image caption Waziri wa Italia akutana na serikali ya Tripoli

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Italia amewasili mjini Tripoli Libya, kwa mazungumzo na kiongozi wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa nchini Libya.

Kiongozi mpya wa serikali inayotambuliwa kimataifa ni Bwana Fayez Seraj.

Paolo Gentiloni, ni afisa mkuu wa kwanza wa bara Ulaya, kufanya ziara rasmi nchini Libya, tangu utawala mpya unaoungwa mkono na Umoja wa mataifa kuwekwa katika mji mkuu wa Libya, majuma mawili yaliyopita.

Obama ajutia makosa ya Marekani nchini Libya

Italia - iliyoitawala zamani Libya katika enzi za ukoloni - kwa pamoja na mataifa kadhaa ya dola za kimagharibi, zimeahidi kuisaidia serikali hiyo mpya, kwa imani kuwa utaleta umoja wa kitaifa na kuwaunganisha raia dhidi ya makundi ya wapiganaji wa Islamic State.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kiongozi mpya wa serikali inayotambuliwa kimataifa ni Bwana Fayez Seraj.

Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa inatazamiwa kuchukua mahala pa serikali pinzani inayoungwa mkono na makundi ya wapiganaji wenye silaha, ambayo ilichipuka mara tu baada ya kuangushwa kwa utawala wa hayati kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.