Huwezi kusikiliza tena

KQ Kupata faida mwakani asema mkurugenzi

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege la Kenya - Mbuvi Ngunze ameiambia BBC kwamba kampuni hiyo itarudi kupata faida katika muda wa mwaka mmoja.

Kampuni hiyo ipo katikati ya mpango wa kuimarisha faida zake kufuatia hasara kubwa za zaidi ya miaka mitatu.

Katika mwaka wa fedha uliopita Kenya Airways ilipata hasara ya zaidi ya dola milioni 250.

Lakini mwishoni mwa juma lililopita ilitajwa kama kampuni ya ndege inayoongoza Afrika katika tuzo ya World Travel Awards, na kuipiku kampuni ya ndege ya Afrika kusini kwa mara ya kwanza katika miaka 20.

Mwandishi wa BBC Anne Soy ametuandalia taarifa hii.