Muendesha mashtaka auawa Musumbiji

Image caption Marcelino Vilankulo, alikuwa akishungulikia kesi inayomhusu mmoja wa watu wanaodaiwa kuhusika na utekaji nyara.

Muendesha mashtaka wa serikali ambaye amekuwa akichunguza misururu ya visa vya utekaji nyara nchini Musumbiji, ameuawa nje ya nyumba yake katika mji mkuu Maputo.

Marcelino Vilankulo, alikuwa akishungulikia kesi inayomhusu mmoja wa watu wanaodaiwa kuhusika na utekaji nyara.

Wengi wa wale wanaotekwa nyara ni wafanyibiashara wa asili ya Asia.

Miaka miwili iliyopita , jaji mmoja alipigwa risasi huko maputo, punde baada ya kuidhinisha kufungwa kwa mfanyibiashara kuhusiana na utekaji nyara.