Mawasiliano ya mitandao yakatwa Oromia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu nchini Ethiopia, hutegemea mtandao wa kampuni ya serikali wa Ethio Telecom ili kuweza kufanya mawasiliano.

Watu katika sehemu tofauti nchini Ethiopia likiwemo eneo linalokumbwa na matatizo la Oromia, wamekuwa hawawezi kutumia mitandao ya kijamii kama vile WhatsApp na Twitter kwa zaidi ya mwezi mmoja kwa mujibu wa shirika la Bloomberg.

Raia wa Ethiopia, hutegemea mtandao wa kampuni ya serikali wa Ethio Telecom ili kuweza kufanya mawasiliano.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Serikali ya Ethiopia imesema kuwa kupotea kwa huduma za mitandao ni kutokana na matatizo ya mawasiliano.

Bloomberg, imenukuu mteja aliyekuwa amegadhabishwa akisema hali hyo inalenga mitandao ya simu .

Maandamano huko Oromia, ya mwaka jana, yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 200 kulingana na kundi la kutetea haki za binadamu,

Serikali ya Ethiopia imeliambia shirika la habari la Bloomberg kwamba kupotea kwa huduma za mitandao ni kutokana na matatizo ya mawasiliano na sio ya kimakusudi