Wanafunzi 62 wafukuzwa chuoni Nairobi

Image caption Chuo cha Nairobi kilikumbwa na ghasia zilizotokana na uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi.

Jumla ya wanafunzi 62 wa chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya wamefukuzwa kutoka chuo hicho, baada ya kushuhudiwa ghasia zilizosababisa kufungwa kwa chuo kwa muda usio julikana wiki moja iliyopita.

Wanafunzi waliteketeza kwa moto afisi za chuo hicho kutokana na kile kinachotajwa kuwa matokeo ya uchaguzi wa kumchagua kiongozi wa wanafunzi chuoni.

Chuo kikuu cha Nairobi kiliseme kuwa kilichukua hatua hizo za kinidhamu dhidi ya wanafunzi walioshiriki katika kuharibu mali ya umma.