China yawazuia raia wa Taiwan

Haki miliki ya picha
Image caption China imesema kuwa watu hao wanashukiwa kufanya ulaghaina kusababisha hasara kubwa kwa watu nchini humo.

China imesema kuwa inazuilia raia wa Taiwan baada ya kuwashuku kuhusika katika ulaghai wa kwa njia ya kielektroniki dhidi ya watu nchini China.

Raia hao wa Taiwan walikuwa wameondolewa mashtaka ya ulaghai nchini Kenya.

Kenya imekuwa ikiwatimua watu hao na kuwapeleka nchini China badala ya Taiwan hatua ambayo imeikasirisha Taiwan.

Maafisa nchini China wamesema kuwa watu hao wanashukiwa kufanya ulaghai kupitia simu na kusababisha hasara kubwa ya kifedha kwa watu China.

Taiwan nayo imeishutumu China kwa kuwateka nyara raia wake.