Mwanajeshi wa Ufaransa auawa nchini Mali

Image caption Kuna takriban wanajeshi 3500 wa Ufaransa eneo la Sahel

Mwanajeshi wa Ufaransa ameu\wa wakatai wa oparesheni ya kijeshi kaskazini wa Mali.

Mwanajeshi huyo aliuawa na bomu la kutegwa ardhini alipokwa akisafiri akitumia gari la kijeshi kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya rais.

Wizara ya ulinzi ilisema kuwa msafara huo wa magari , ulikuwa ukielekea eneo la kaskazini kutoka mji wa Gao kwenda Tessalit wakati bomu hilo lililipuka.

Wanajeshi wengine watatu waliokuwa ndani ya gari hilo nao walijeruhiwa.

Takriban wanajeshi 3500 wa ufaransa wako kwenye nchi tano za eneo la Sahel. katika oparesheni inayoongozwa na ufaransa dhidi ya makundi ya wanamgambo iliyoanza mwaka 2014.