Benzema hatoshiriki Euro2016- FFF

Haki miliki ya picha AP
Image caption Benzema hatoshiriki Euro2016 asema kocha Deschamps

Mshambulizi wa Real Madrid na Ufaransa Karim Benzema, amepigwa marufuku ya kutoshiriki mashindano ya Euro2016 yanayotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

Shirikisho la soka la Ufaransa FFF limesema kuwa hakuna pingamizi kisheria linalomzuia mshambuliaji huyo asishiriki kindumbwendumbwe hicho ila kunahofu uwepo kwake katika timu ya taifa huenda ukahujumu mtagusano.

Aidha FFF linasema kuwa kuwepo kwake hakutatoa picha nzuri kwa mamilioni ya watu wanaomtazama.

Benzema alipigwa marufuku mwezi Desemba mwaka uliopita baada ya kupatikana na hatia ya

Mshambuliaji huyo anachunguzwa kwa madai kwamba alihusika katika njama ya kutishia na kudai pesa kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Ufaransa Mathieu Valbuena.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nyota huyo wa Real Madrid amekanusha madai hayo.

Nyota huyo wa Real Madrid amekanusha madai hayo.

Kocha wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps,ameiambia shirikisho la FFF kuwa anahofia Benzema ataidhuru motisha ya timu yake.