Riek Machar awasili Sudan Kusini

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Machar alikuwa katika makao makuu ya waasi yaliyo katika mji wa Pagak

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar, amerejea nchini humo huku akitarajiwa kuchukua majukumu yake mapya kama Makamu wa Rais wa Kwanza.

Bw Machar anatarajiwa kufika mji mkuu Juba Jumatatu tarehe 18 Aprili.

Msemaji wake amethibitisha kwamba Bw Machar alikuwa katika makao makuu ya waasi yaliyo katika mji wa Pagak mpakani na taifa jirani la Ethiopia.

Baadhi ya waasi tayari wamewasili mjini Juba, na akizungumza punde baada ya kuwasili, naibu kiongozi wa waasi Alfred Ladu Gol amesema wakati umewadia kwa raia wote wa taifa hilo kuungana na kufanya kazi kwa pamoja.