Mataifa ya OEC yakutana Ufaransa

Image caption OEC

Maafisa wa mamlaka ya za ushuru kutoka mataifa wanachama wa shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo OEC wako mjini Paris Ufaransa hivi leo kubuni njia mwafaka za kukabiliana na tatizo la ukwepaji wa kulipa kodi duniani.

Mkutano huo umeandaliwa baada ya kufichuliwa kwa nyaraka za siri kutoka kwa kampuni ya mawakili ya Mossack Fonseca nchini Panama.

Australia, ambayo iliitisha kikao hicho imesema kuwa inatumai mataifa yatakubali kubadilishana taarifa na kubuni mbini za ushirikiano katika siku zijazo.

Haki miliki ya picha
Image caption Polisi walivamia ofisi za Mossack Fonseca

Nchini Panama mawakala kutoka afisi ya mkuu wa sheria wamevamia jengo la kampuni ya mawakili ya Mossack Fonseca, kutafuta ushahidi wowote unaohusiana na biashara haramu.

Kampuni hiyo imeshutumiwa kwa kuepuka kulipa kodi na ulaghai lakini mwanzilishi wake Ramon Fonseca amesema kuwa operesheni zake zote ni halali.