Mbwa wa Manchester watambua tamutamu pekee

Wanyama Haki miliki ya picha PA
Image caption Mbwa hao waligundua tamutamu na nyara ya pori

Ripoti moja inasema kwamba mbwa wa kunusa katika uwanja wa Manchester Uingereza wamekosa kugundua mihadarati katika kipindi cha miezi saba.

Hata hivyo mbwa hao wanaweza kunusa tamu tamu kama vile jibini na soseji kutoka kwenye mikoba ya wageni wanaofika kwenye uwanja huo.

Mbwa hao sita wanaogharimu dola milioni mbili za Kimarekani kuwatunza walipata mafunzo ya kutambua mihadarati, tumbaku, pesa, nyama ya pori.

Hata hivyo kwa kipindi cha miezi saba maafisa wa uhamiaji wamesema walishindwa kupata dawa za kulevya aina ya kokeini na heroini.

Ripoti hii inapendekeza matumizi ya mbwa hao yabadilishwe.