Upinzani waandamana Zimbabwe

Image caption Kiongozi wa MDC Morgan Tsvangirai

Karibu wafuasi 2000 wa upinzani nchini Zimbabwe wamekuwa wakifanya maandamano katika mji mkuu Harare, kulalamikia kuendelea kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo.

Waandamanaji hao waliongozwa na kiongozi wa chama cha (Movement for Democratic Change) Morgan Tsvangirai.

Image caption Waandamanaji wanalalamikia kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo.

Wengi walibeba mabango wakimtaka rais wa Zimbabwe Robert Mugabe , mwenye umri wa miaka 92 ajiuzulu.

Polisi wa kupambana na ghasia walifunga barabara za kuelekea majengo ya bunge ya nchi hiyo.