Waziri wa uchukuzi ajiuzulu Ubelgiji

Haki miliki ya picha Horst Pilger
Image caption Uwanja wa ndege ulioshambuliwa Brussels

Waziri wa uchukuzi nchini ubelgiji Jacqueline Galant amejiuzulu, baada ya ripoti ya kisiri ya muungano wa Ulaya, kufichua dosari za usalama kwenye viwanja vya ndege kufuatia mashambulizi ya mwezi uliopita ya kujitoa mhanga mjini Brussels.

Ripoti hiyo ya muugano wa ulaya ya tangu mwaka uliopita ilitolewa kwa umma na vyama viwili vya upinzani nchini Ubelgiji.

Ilisema kuwa huduma za usalama katika viwanja vye ndege nchini ubelgiji zina dosari na kutilia shaka jinsi ukaguzi unavyofanywa.