Kura ya kumtimua Rousseff itafanyika

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Rousseff amelaumiwa kwa kuvuruga bajeti kabla ya uchaguzi wa mwaka 2014.

Mahakama ya juu zaidi nchini Brazil imekataa ombi la serikali ya kutaka kutupiliwa mbali kura ya bunge kuamua ikiwa rais Dilma Rousseff ataondolewa madarakani.

Mahakama imekataa kufuta amri ya kupiga kura iliyoamuliwa na spika wa bunge la chini, ambayo itaamua siku ya Jumapili ikiwa Rousseff ataondolewa madarakani.

Wafuasi wa rais walikuwa wamedai kuwa zoezi hilo litavurugwa kwa sababu wabunge kutoka majimbo yanayompinga Rousseff. huenda wakapiga kura kwanza.

Bi Rousseff amelaumiwa kwa kuvuruga bajeti kabla ya uchaguzi wa mwaka 2014 madai ambayo anayapinga.