Sarafu ya Zambia yafanya vyema duniani

Haki miliki ya picha
Image caption Kiwanda cha shaba nchini zambia

Sarafu ya Zambia ya Kwacha ndiyo sarafu iliyo na biashara nzuri zaidi duniani mwaka 2016, kwa mujibu wa shirika la habari la Bloomberg.

Shirika hilo linasema kuwa thamani yake dhidi la dola ya marekani imepanda kwa asilimia 19.9 tangu mwezi Januari.

Hii inajiri baada ya sarafu hiyo kuorodheshwa kwa kuwa moja ya sarafu zilizokuwa na biashara duni zaidi duniani mwaka uliopita.

Image caption Huenda kwacha ikaboreka zaidi dhidi ya dola

Hali hii ilitokana na kushuka kwa bei ya shaba nyekundu ambayo ndiyo moja ya bidhaa muhimu inayouzwa nje pamoja na kuwepo uhaba wa nishati.

Bloomberg imenukuu wadadisi wakisema kuwa sarafu ya Kwacha itazidi kuboreka wakati bei ya shaba inaimarika.