Majambazi yasumbua jimboni Punjab

Jeshi nchini Pakistan wameamua kutumia chopa katika makabiliano ya bunduki katika operesheni maalum ya kukabiliana na genge la majambazi kutoka katika maficho yao yaliyoko karibu na mto Indus jimboni Punjab.

Maofisa wa polisi wameelezea hali ya mapigano makali ya kurushiana risasi yanaendelea eneo la tukio ikiwemo miripuko ya mabomu na makombora imekuwa ikisikika,kutokana na hali hiyo amri ya hali ya hatari imeweka katika baadhi ya maeneo kwenye jimbo hilo.

Jeshi lilichukua uamuzi wa kupambana na genge hilo la majambazi mwishoni mwa wiki hii baada ya genge hilo lijulikanalo kama "Chotu gang" kuwaua polisi sita na kuwateka nyara polisi wengine ishirini na wanne .

Genge hilo limekuwa likishutumiwa kwa utekaji nyara wa maelfu ya watu na matukio mengine ya uhalifu katika miaka ya hivi karibuni.