Annan: Nkurunziza hakustahili kuwania urais

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Annan: Nkurunziza hakustahili kuwania urais

Aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa bwana Kofi Annan amemkosoa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwa kuwania muhula wa tatu.

Bw Annan amesema Nkurunziza anafahamu vyema kuwa ni kinyume cha katiba ya taifa hilo kuwania madaraka kwa zaidi ya vipindi viwili.

Haki miliki ya picha
Image caption Raia huyo wa Ghana anamlaumu rais Nkurunziza kwa kusababisha maandamano yaliyosababisha vifo vya takriban watu mia nne

Raia huyo wa Ghana anamlaumu rais Nkurunziza kwa kusababisha maandamano yaliyosababisha vifo vya takriban watu mia nne.

Bw Annan ameiambia BBC kuwa bw Nkurunziza haoneshi dalili zozote za kutafuta suluhu la amani wala nia ya kutaka mazungumzo ya kweli na wapinzani wake.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bw Annan ameiambia BBC kuwa bw Nkurunziza haoneshi dalili zozote za kutafuta suluhu la amani

Katibu huyo wa zamani ameiomba jamii ya imataifa kuyasaidia mataifa ya Afrika yanayokabiliwa na matatizo chungu nzima kama vile Ethiopia inayokabiliwa na baa la njaa

Annan anasema kuwa mataifa hayo ya Afrika yamesahaulika huku kurunzi ya ulimwengu ikiangazia Syria na mataifa ya Mashariki ya kati.