Watu 233 wamethibitishwa kufariki Ecuador

Haki miliki ya picha AP
Image caption Idadi ya wahasiriwa Ecuador imetimia 233

Idadi ya watu waliothibitishwa kufariki kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Ecuador imegonga 233 na kunahofu idadi hiyo itaongezeka maradufu.

Rais wa taifa hilo Rafael Correa amesema katika hotuba fupi kuwa wanajeshi elfu kumi (10,000) wametumwa kusaidia na shughuli za uokozi.

Aidha Polisi 3,500 pia watajiunga nao kusaidia kuokoa maisha ya majeruhi wa janga hilo la kitaifa.

Tetemeko hilo kubwa lililotikisa maeneo ya Kusini mwa pwani ya Ecuador lilikuwa la kiwango cha 7.8 kwenye vipimo vya Richter.

Image caption Kitovu chake kilikuwa takriban kilomita 27 kutoka kwa mji wa pwani uitwao Muisne mji ambao kwa kawaida hauna wakaazi wengi.

Makamu wa rais wa nchi hiyo ametangaza hali ya tahadhari katika mikoa sita nchini humo, huku maafisa wa huduma za dharura wamepelekwa kusaidia .

Kitovu chake kilikuwa takriban kilomita 27 kutoka kwa mji wa pwani uitwao Muisne mji ambao kwa kawaida hauna wakaazi wengi.

Maafisa wakuu wanahofia kuwa idadi hiyo ya vifo huenda ikaongezeka kwani maeneo ya mashambani mbali na kitovu cha tetemeko hilo yaani mji wa pwani wa Muisne ndiyo yameanza kutoa taarifa kwa vyombo vya dola kuhusu athari ya tetemeko hilo.

Maafisa katika kituo cha Marekani cha utafiti wa kijiologia wamesema tetemeko hilo la ardhi lilitikisa hadi sehemu ya mpakani na taifa jirani ya Colombia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Correa amewahakikishia wahasiriwa wa mkasa huo kuwa msaada wa serikali uko njiani.

Rais Correa amewahakikishia wahasiriwa wa mkasa huo kuwa msaada wa serikali uko njiani.

Hata hivyo mabasi na malori ya kijeshi yanatatizika kuwafikia wahanga walioporomokewa na majengo yao kufuatia maporomoko makubwa ya ardhi yaliyoziba mabarabara.

Aidha misaada ya chakula na madawa kutoka mataifa jirani yameanza kupokewa kutoka Venezuela na Mexico.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Takriban watu 600 wamejeruhiwa japokuwa idadi hiyo bila shaka inatarajiwa kupanda.

Takriban watu 600 wamejeruhiwa japokuwa idadi hiyo bila shaka inatarajiwa kupanda.

Meya wa mji wa Pedernales Gabriel Alcivar,ameiambia BBC kuwa mji wote umeporomoka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meya wa mji wa Pedernales Gabriel Alcivar,ameiambia BBC kuwa mji wote umeporomoka.

Mji wa Guayaquil ulioko takriban kilomita 300km kutoka kitovu cha tetemeko hilo pia limeathirika vibaya na hata daraja la pekee linaloiunganisha limeporomoka.

Visa vya utovu wa nidhamu pia vimeripotiwa huku watu wakipora majengo ya watu na maduka.