Haki za binaadamu ziheshimiwe, Francois Hollande

Image caption Francois Hollande

Raisi wa Ufaransa Francois Hollande,ameitembelea Misri na kusisitiza kuwa haki za binadamu zinapaswa kuheshimiwa kwa kuwa sio kikwazo katika kupambana na ugaidi lakini ni msaada mkubwa katika kupambana nao.

Hollande alitoa rai hiyo baada ya mazungumzo baina yake na kiongozi wa Misri Abdel Fattah al-Sisi,ambaye alikosolewa kwa kutozingatia haki za binadamu.

"Haki za binadamu ni suala ambalo halina kipingamizi,lina mianya ya kupinga ugaidi pale ambapo ulinzi upo na hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaokiuka.Haki za binadamu ni sawa na uhuru wa habari,uhuru wa kujieleza na vilevile kuwa na mfumo wa mahakama ambao utaweza kujibu kila swali , anasema Francois"