Ukame waitesa Afrika

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kofi Annan Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Afrika

Katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa,Kofi Annan ameitaka dunia kutoa misaada ya kifedha kwa nchi za Afrika kama Ethiopia ambazo zinateseka na ukame,Kofi amesema dunia imejisahau kwa kuweka kipaumbele kwa nchi ya Syria na mashariki ya kati wakati nchi zingine zikiteseka.

"Kuna mazoea ambayo jumuiya za kimataifa zimejiwekea kwa muda kwa kutoa kipaumbele kwa janga moja na kusahau jingine.Hivyo ombi langu kwa jumuiya ya kimataifa ni kuwa na huruma na watu wanaohitaji chakula na kuunga mkono jitihada za shirika la chakula duniani WHO, na mashirika mengine ya misaada."