Myanmar yawaachia wafungwa wote wa kisiasa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafungwa wa kisiasa 83 nchini Myanmar wameachiwa huru.

Wafungwa wa kisiasa 83 nchini Myanmar wameachiwa huru.

Serikali mpya ya Myanmar ya Bi Aung San Suu Kyi inayongozwa na rais Htin Kyaw imeamuru kuachiwa kwa kundi la pili kubwa la wafungwa wa kisiasa nchini humo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Aung San Suu Kyi alitangaza nia ya kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa

Kundi la wafungwa wapatao 100 waliachiliwa huru mapema mwezi huu.

Maafisa wamesema hatua hiyo ya kuwaachia wafungwa wa kisiasa ambayo ni miongoni mwa maaamuzi makuu ya kwanza yaliyoanza kutekelezwa na serikali ya Bi San Suu Kyi's, itaendelea