Bei ya mafuta yaporomoka Iran

Haki miliki ya picha EPA

Bei ya mafuta imeshuka ghafla nchini Iran, baada ya wasambazaji wakuu kushindwa kukubaliana katika mipango ya kusimamisha uzalishaji ili kuweza kupunguza kasi ya usambazaji wa mafuta hayo.Ndani ya saa chache,bei ya mafuta ilishuka kwa Zaidi ya asilimia tano.

Wazalishaji wa mafuta walikuwa na matumaini ya kuongeza bei lakini maongezi hayo yalisababisha mgogoro kwa Iran ,nchi ambayo ndio soko linalotegemewa.

Saudi Arabia haikutaka kujitoa katika uzalishaji labda kama Iran itakubaliana kufanya sawa na wao ingawa Wairani wanataka kuuza mafuta Zaidi ili kunufaika Zaidi kimataifa.