Iran yakataa kudhibiti uzalishaji mafuta

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Iran yakataa kudhibiti uzalishaji mafuta

Mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi duniani yanakutana katika mji mkuu wa Qatar Doha kujaribu kuafikiana kupunguza kiwango cha uzalishaji bidhaa hiyo adimu kwa lengo la kuimarisha bei. Miongoni mwa mataiafa yaliokatika mstari wa mbele kutaka viwango vya uzalishaji vipunguzwe ni Saudi Arabia na Urusi.

Hata hivyo Iran, moja ya mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi imesusia mkutano huo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi duniani yanakutana katika mji mkuu wa Qatar Doha kujaribu kuafikiana kupunguza kiwango cha uzalishaji

Waziri wa mambo ya nje wa Iran anasema maafikiano ya kupunguza uzalishaji yatazuia nchi yake kufaidi kutokana na mauzo ya bidhaa zake za mafuta ...ikizingatiwa kuwa walikuwa wamefungiwa soko kwa mda mrefu kutokana na vikwazo vya kiuchumi walivyokuwa wamewekewa.

Bei ya mafuta imekuwa ikidorora na sasa ni nusu ya ilivyokuwa miaka miwili iliyopita hivyo kuathiri pakubwa uchumi wa mataifa husika.

Chumi za mataifa yanayotegemea uuzaji wa mafuta zimedorora na hivyo kutoa haja ya kupunguza uzalishaji angalau kuimarisha baei ya mafuta katika soko la dunia.