Papa Francis atetea mkutano na Bernie Sanders

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Papa Francis atetea mkutano na Bernie Sanders

Papa Francis ametetea vikali hatua yake ya kukutana na mgombea wa tikiti ya urais katika chama cha Democratic Bernie Sanders.

Kuhusu tetesi kwamba hatua hiyo ni kuingilia siasa za Marekani ,amejibu kwa mas-hara akisema kwamba..., aliye na fikra hizo anashauriwa kumuona daktari wa maswala ya kisaikologia.

Pope Francis na Bwana Sanders walikutana kwa mda mfupi baada ya Sanders kuhutubia mkutano kuhusu haki za kijamii huko Vatican.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bw. Sanders anawania tiketi ya chama cha Democratic

Bw. Sanders anawania tiketi ya chama cha Democratic dhidi ya mpinzani wake anaeongoza katika kinyanganyiro hicho Bi Hillary Clinton .

Bila shaka mkutano huo utamuongezea sifa bw. Sanders, hasa wakati huu ambapo zimebaki siku mbili tu kabla ya kura ya mchujo ya jimbo kubwa na muhimu la New York.