Wayemeni wa Guantanamo wapelekwa Saudia

Haki miliki ya picha United States Department of Defense
Image caption Wayemeni wa Guantanamo wapelekwa Saudia

Makao makuu ya jeshi la Marekani Pentagon, imesema wafungwa 9 wa Yemeni waliokuwa wakizuiliwa katika gereza la Guantanamo Bay sasa wamehamishiwa nchini Saudi Arabia.

Maafisa wa Marekani wanasema wameamua kuwapeleka wafungwa hao Saudia kwa sababu Yemen ingali inakabiliwa na mzozo wa kisiasa, na pia baadhi ya wanafamilia wao wako Saudia.

Mmoja wa wafungwa hao ni yule aliyekuwa akitumia njia ya kususia chakula mda mrefu akipinga kuzuiliwa kwake.

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Obama anataka kulifunga gereza hilo la Marekani lililoko Guantanamo Cuba.

Kundi hili likishaondoshwa , Wafungwa 80 ndio idadi ya watakaosalia huko Guantanamo ambako wamekuwa wakizuiliwa pasi na kufunguliwa mashtaka kwa mda wa zaidi ya miaka 10 iliyopita. .

Rais Obama anataka kulifunga gereza hilo la Marekani lililoko Guantanamo Cuba.