Tetemeko laacha maafa Equador

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Matokeo ya tetemeko Ecuador

Serikali nchini Ecuador imethibitisha kuwa takribani watu 413 wamefariki Dunia kutokana na tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo.Hata hivyo idadi inayotajwa ya watu waliokufa ni kwa siku ya jumamosi tu.

Tetemeko hilo pamoja na kusababisha idadi hiyo kubwa ya vifo lakini zaidi ya watu 2000 wamejeruhiwa pia.

Rais wa Ecuado Rafael Correa amesema kuwa hili ni moja ya janga kubwa kuwahi kulikumba taifa hilo ndani miongo saba iliyopita katika pwani ya Pacific na kuharibu miundo mbinu na makazi.

Kikosi cha waokoaji na Polisi wapatao 14,000 wametumwa katika eneo lililokumbwa na tetemeko hilo kwaajili ya uokoaji kuwasaidia waliopoteza makazi yao na ambao bado wapo katika mazingira ya hatari.

Waokoaji hao wanatumia ndege na kwenda moja kwa moja katika maeneo ya utoaji msaada.