Waliotarajia Mugabe aanguke waambulia patupu !

Image caption Afya ya rais Mugabe imekuwa ikidhohofika katika miaka ya hivi karibuni

Je unaikumbuka picha hii ?

Haya basi , Maafisa wa usalama wa kitengo cha kumlinda rais wa Zimbabwe Robert Mugabe walilazimika kumsogelea kwa karibu mno kiongozi huyo mkongwe katika tukio lililowaudhi raia wengi waliofika katika uwanja wa kitaifa jijini Harare kwani hata wenyewe hawakuweza kumtazama ''baba wa taifa''

Yamkini kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 92 aliingia katika uwanja wa kitaifa akiwa kwenye gari rasmi la Kijeshi

Image caption Maafisa wa usalama wa kitengo cha kumlinda rais wa Zimbabwe Robert Mugabe walilazimika kumsogelea kwa karibu mno

Hata hivyo baada ya kukagua gwaride la jeshi maafisa hao wa usalama walipanga kikamilifu njia ya kumstiri rais Mugabe asije akakungua na kuanguka kama ilivyokuwa mwaka uliopita

Bw Mugabe alikuwa akiongoza taifa katika kuadhimisha miaka 36 ya uhuru kutoka kwa minyororo ya ukoloni.

Rais Mugabe aliwaomba radhi wafanyikazi wa serikali waliostaafu kwa kuchelewa kupata malimbikizi ya marupurupu yao

Image caption Bw Mugabe alikuwa akiongoza taifa katika kuadhimisha miaka 36 ya uhuru

''Bila shaka malipo yenu na mishahara ya siku za usoni itawafikia kwa muda ufaao'' alisema rais Mugabe.

Mugabe aliwataka wazimbabwe waache ukabila na ufisadi iwapo wanaitaka Zimbabwe iimarike kiuchumi tena.

Taifa hilo limekumbwa na udhaifu wa sarafu yake baada ya sera ya serikali ya kuwapokonya wakoloni wazungu mashamba na kisha kuyagawanyia waafrika weusi ambao ndio wengi kukosolewa vikali na mataifa ya magharibi yakongozwa na Uingereza.