Tamasha la Ivor Novella lampuuza Adele

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Adele

Mwanamuziki mashuhuri Adele ameshindwa kupata uteuzi katika tamasha la kuwatuza wasanii la Ivor Novello ambalo hutambua ufanisi wa uandishi wa nyimbo.

Nyota huyo ambaye albamu yake ya tatu iliuza sana mwaka 2015,hakuangaziwa katika tuzo hizo ambazo hupigiwa kura na watunzi pamoja na waandishi wa nyimbo.

Badala yake Ed Sheen,Jess Glynne na James bay waliorodheshwa kuwania tuzo hiyo.