Fidel Castro ahutubia Cuba

Image caption Fidel Castro

kiongozi wa awali wa Mapinduzi ya Cuba Mapinduzi, Fidel Castro, ametoa hotuba ya nadra katika siku za mwisho mwisho za utawala wa chama chake cha kikomunisti.

Katika hotuba yake, raisi huyo mstaafu mwenye umri wa miaka themanini na tisa ametoa mfano wa umri wake mkubwa na kutetea utawala wake wa kikomunisti.

Kiongozi mrithi, ambaye ni nduguye mwenye umri wa miaka themanini na minne Raul Castro, amethibitishwa kiongozi mkuu wa chama chake cha kikomunisti kwa muhula wa miaka mingine mitano.

Mwandishi wa BBC aliyejo mjini Havana amesema kwamba tamko hilo litafifiza matumaini ya Wacuba wengi ambayo yalifikiwa hivi karibuni katika mahusiano ya kimataifa na nchi ya Marekani na kueleza kwamba ilikuwa ni ishara ya maandalizi ya wazushi kuchukua hatamu za uongozi.