Fabregas: Wachezaji walimsaliti Mourinho

Mourinho Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mourinho alifutwa kazi Desemba

Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas amesema Jose Mourinho alikosa kufanikiwa Stamford Bridge msimu huu kwa sababu aliwaamini wachezaji kupita kiasi.

Mourinho, 53, alifutwa mwezi Desemba klabu hiyo ikiwa alama moja pekee juu ya eneo la kushushwa daraja.

Jambo la kushangaza ni kwamba miezi mmoja awali, Mourinho alikuwa amewaongoza kushinda taji la Ligi ya Premia.

Fabregas, 28, sasa anasema wachezaji walikosa kufanya hisani baada ya kuongezewa muda wa kukaa likizoni kama zawadi kwa kushinda ligi.

“Namheshimu sana,” Fabregas aliambia Sky Sports.

Haki miliki ya picha Reuters

"Tatizo kubwa ni kwamba alikuwa na imani sana nasi, aliongezea likizo kwa sababu tulikuwa tumeshinda ubingwa lakini hatukumtendea hisani, tulimsaliti.

"Hiyo ndiyo sababu kuu akafutwa, na kwa sababu ya hilo mimi na wachezaji wengine katika timu tunajilaumu.”