Msumbiji mashakani kwa kuficha madeni yake

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkurugenzi mkuu wa IMF Christine Lagarde

Shirika la fedha duniani IMF, limesitisha ufadhili wake kwa serikali ya Mozambique, baada ya kugundua kuwa serikali ya nchi hiyo ilikosa kutangaza kuwa ilikuwa na madeni ya zaidi ya dola bilioni moja.

Afisa mmoja wa shirika hilo la IMF amesema wafadhili wengine huenda nao wakasitisha ufadhili wao kwa Mozambique.

Hatua hiyo sasa itashinikiza serikali ya Mozambique ambayo hutegemea misaada ya kigeni kufadhili robo moja ya bajeti yake.

Taifa hilo linakumbwa na matatizo ya kiuchumi, yaliosababishwa na kupungua kwa hazina yake ya fedha za kigeni na kushuka kwa dhamana ya sarafu ya nchi hiyo.