Leo ni kivumbi New York

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wagombea wa Democrat Hillary Clinton na Bernie Sanders.

Wagombea waliobaki kwenye kinyanganyiro cha kuwania urais nchini Marekani, wanang'ang'ania kura muhimu zaidi za mchujo hii leo katika jimbo la New york. Likiwa moja ya majimbo makubwa nchini Marekania lina ushawishi mkubwa kwa wagombea wote.

Kwa wagombea wa chama cha Democtrats Bernie Sanders amelelewa mjini New York naye Hillary Clinton amekuwa seneta katika jimbo hilo.

Kwa upande wa Republican mgombea mkuu Donald Trump ni mwenyeji wa jimbo hilo.

Ananuia kupata ushindi dhidi ya mshindani wake mkuu Ted Cruz, Lakini amekosoa mbinu ya kumchagua mgombea wa chama.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wagombea wa Republican Donald Trump na Ted Cruz

Wagombea hao wote wamekuwa kwenye kampeni ya kuwarai wapiga kura. Clinton aliwaambia wapiga kura kuwa hatachukulia chochote kwa msaha huku kwa upande wa Republican Trump akisisitiza mapenzi yake kwa jimbo la New York.

Mshindani wake mkuu Ted Cruz hatarajiwi kufanya vyema baada ya kukosoa sera za Trump mapema kwenye kampeni.