Msomi avua nguo kwa kufungiwa ofisi

Image caption Stella Nyanzi alikuwa akimuunga mkono mgombea urais Kizza Besigye

Hatua ya mwanamke mmoja msomi ya kuvua nguo nchini Uganda imezua mjadala mkali nchini humo.

Baada ya kukerwa na hatua ya kufungiwa nje ya ofisi yake na usimamizi wa chuo kikuu cha Makerere, Stella Nyanzi alivua nguo zote kama njia ya kupinga.

Hata hivyo mwishowe aliruhusiwa kuingia ofisini mwake. Wengi wa wafuasi wake wanasema kuwa alilazimishwa kufanya hivyo kutoka na yake alikuwa akitendewa.

Hata hivyo wale wanaomkosoa wanasema kwa amekiuka maadili na kwamba mwanamke hastahili kuwa uchi hadharani.

Gazeti la the New Vision nchini humo linasema kuwa waziri anayehusika na maadili anataka Nyanzi akamatwe.