Ghasia: Maduka ya raia wa Rwanda yaporwa Zambia

Image caption Ramani ya Zambia

Zaidi ya watu 200 wamekamatwa katika mji mkuu wa Zambia Lusaka huku maandamano ya ghasia na wizi ukiendelea kwa siku ya pili mfululizo.

Makumi ya maduka yanayomilikiwa na raia wa Rwanda yameporwa kufuatia madai kwamba raia wa Rwanda wamekuwa wakishiriki katika mauaji ya kishirikina.

Takriban watu saba wameuawa katika wiki za hivi karibuni na viungo vyao vya mwili kukatwa.

Inadaiwa kwamba viungo hivyo hutumika kufanyia uchawi.

Kuna zaidi ya wakimbizi 7000 wa Rwanda nchini Zambia.

Wengi wao wamedaiwa kutoroka maduka yao na makaazi.