Benki ya Chase kufunguliwa tena Kenya

Benki
Image caption Matawi ya benki hiyo yatafunguliwa Jumatano wiki ijayo

Benki kuu ya Kenya imetangaza kufunguliwa tena kwa benki ya Chase ambayo ilifungwa na kuweka chini ya mrasimu wiki chache zilizopita.

Gavana wa benki kuu ya Kenya ametangaza kuwa matawi yote 62 ya benki hiyo, yatafunguliwa tena ifikapo tarehe 27 mwezi huu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Benki ya Chase ilifungwa na kuweka chini ya mrasimu

Wateja wa benki hiyo wataruhusiwa kutoa hadi shilingi milioni moja baada ya kufunguliwa kwa benki hiyo.

Benki ya Kenya Commercial itachukua asilimia kubwa ya hisa za benki ya Chase na itaongoza shughuli za kuifanyia mabadiliko benki hiyo.