Urusi kuiangukia IAAF

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Vladmir Putin wa Urusi, akimsikiliza waziri wa michezo Vitaly Mutko wakati walipokitembelea kituo cha michezo.

Urusi imetangaza hatua yake ya kutaka kuushawishi uongozi wa chama cha riadha wa dunia ili wachezaji wake waruhusiwe kushiriki katika mashindano ya Olympic Rio mwaka ujao.

Waziri wa michezo,Vitaly Mutko amesema kuwa kwa wale wote wenye nia ya kushiriki michuano hayo lazima wakubali kufanyiwa vipimo vya kuchunguza matumizi ya dawa za kusisimua mara tatu kwa hiari yao.

Shirikisho la riadha la Urusi limeondolewa kwa muda kutoka katika mashindano ya kimataifa, ikiwemo michezo ya Olimpiki, kwa tuhuma za kuhusika katika matumizi ya dawa za kusisimua misuli.