Kanali wa jeshi auawa Burundi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ghasia zilizokuwa nchini Burundi

Kanali mmoja wa jeshi amepigwa risasi na watu wasiojulikana katika mji mkuu wa Burundi ,Bujumbura,kulingana na vyombo vya habari vya kundi la SOS nchini humo.

Kanali Emmanuel Buzubona aliuawa pamoja na mtu mmoja aliyekuwa akiendesha pikipiki siku ya Jumatano kaskazini mwa makaazi ya mji huo.

Ni miongoni mwa maafisa wa jeshi wa hivi karibuni kuuawa tangu rais Pierre Nkurunziza kunusurika jaribio la mapinduzi na maandamano kufuatia hatua yake ya mwaka jana kujiongezea mda wa kuhudumu kama rais wa taifa hilo.