Mpango wa Fifa kumsihi Nkurunziza kujiuzulu

Image caption Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi

Aliyekuwa rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter ameelezea vile maafisa wa serikali ya Uswizi walivyomtaka kumsihi rais wa Burundi anayependa soka Pierre Nkurunziza kujiuzulu kufuatia maandamano dhidi ya uongozi wake mwaka uliopita,kulingana na jarida la soka duniani.

Madai hayo yameandikwa katika wasifu wa Seppo Blatter kwa jina Mission & Passion, Fussball ambalo limechapishwa nchini Ujerumani .

Mnamo mwezi Mei ,waziri wa kigeni wa Uswizi Yves Rossier alimtaka Sepp Blatter kumpatia Nkurunziza kazi ya ubalozi wa soka kulingana na jarida hilo.

Bwana Rossier alifanya ombi hilo baada ya kuagizwa na Marekani,lakini mpango huo ukafeli kwa sababu alikuwa na maswala mengine yaliokuwa yakimkabili,bwana Blatter alinukuliwa akisema.