Canada kuhalalisha matumizi ya bangi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Canada

Serikali ya Canada itabuni sheria mwaka ujao ambazo zitahalalisha uuzaji wa bangi.

Iwapo sheria hiyo itaidhinishwa ,italiorodhesha taifa la Canada miongoni mwa mataifa yenye uchumi mkubwa magharibi kukubali utumizi wa bangi.

Waziri mkuu Justin Trudeau alipigania dawa hiyo kuhalalishwa wakati wa kampeni.Waziri wake wa afya amesema kuwa anataka dawa hiyo kutowafikia watoto pamoja na wahalifu.

Serikali imeahidi kufanya kazi na maafisa wa polisi ili kuwadhibiti wale wanaouziwa dawa hiyo,wakati inapouzwa na vile inavyotumiwa na wametafuta njia ya kudhibiti dawa hiyo kupitia sheria za uuzaji wa pombe.

Hatahivyo wapinzani wanasema kuwa hatua mbaya zaidi kwa vijana ni kuruhusu utumiaji wa dawa hiyo ya kulevya.

Utumizi wa bangi nchini humo utasalia kuwa marufuku huku sheria za kuhalalisha zikiendelea kutengezwa.