Uhusiano wa Malkia Elizabeth na Afrika Mashariki

Elizabeth Haki miliki ya picha EPA
Image caption Malkia Elizabeth alizaliwa tarehe 21 Aprili, 2016

Malkia Elizabeth wa Uingereza, ambaye alitimiza umri wa miaka 90 Alhamisi, amekuwa na uhusiano wa karibu na nchi za Afrika Mashariki. Alipashwa habari kwamba amekuwa malkia akiwa Kenya, na pia amekutana na raia wa Tanzania na Uganda.

Huu hapa ni mkusanyiko wa picha zinazoeleza uhusiano huu.

Haki miliki ya picha Getty

1. Hapa Malkia Elizabeth, wakati huo akiwa Bintimfalme, anawapungia wananchi mkono kutoka ukumbi wa baraza la jiji tarehe 4 Februari, 1952 akiwa na Mwanamfalme Philip, ambaye ni mumewe na Msimamizi wa Edinburgh. Babake, Mfalme George IV alifariki Malkia Elizabeth akiwa likizoni Kenya

2. Alirejea Uingereza baadaye mwezi huo na kutua kwa mara ya kwanza kama Malkia nchini Uingereza.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Arejea Uingereza kama Malkia

3. Alizuru Kenya baadaye. Hapa ni mwaka 1983 akikagua gwaride la heshima katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta.

Haki miliki ya picha PA

4. Amewahi pia kuzuru Uganda. Picha hii inamuonesha akiwa kituo cha Mildmay cha kuwatunza mayatima waliofiwa na wazazi wao kutokana na Ukimwi 22 Novemba, 2007 mjini Kampala. Baadaye alifungua mkutano wa viongozi wa nchi za Jumuiya ya Madola uliokuwa ukifanyika mjini Kampala.

Haki miliki ya picha Getty

5. Malkia Elizabeth huendesha mpango wa kuwawezesha viongozi vijana wa The Queen's Young Leaders. Hapa anaonekana akizungumza na Mkenya Caren Nelima Odanga (kwanza kushoto) na Angela Benedicto Mnagoza kutoka Tanzania (pili kushoto) wakati wa dhifa ya kuwapokea viongozi vijana kutoka nchi za Jumuiya ya Madola kasri la Buckingham Palace jijini London Juni 22, 2015.

Haki miliki ya picha Getty

Mpango huo hufaidi viongozi vijana wa umri wa kati ya miaka 18 na 29.

6. Mabalozi wa nchi za Afrika Mashariki nchini Uingereza ni baadhi ya viongozi waliofanikiwa kukutana na Malkia Elizabeth. Huyu hapa ni Lazarus Amayo aliyekutana na Malkia 12 Machi 2015.

Haki miliki ya picha Getty