Volkswagen kununua magari yake

Haki miliki ya picha
Image caption Matthias Mueller Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya utengenezaji magari ya Volkswagen

Kampuni ya magari ya Volkswagen imetangaza kuyanunua magari ya kampuni yake kutoka kwa wateja nchini Marekani yapatayo nusu milioni kama sehemu ya kutimiza makubaliano yaliyofikiwa na idara ya sheria ya Marekani dhidi ya makampuni ya kutengeneza na kashfa ya uchafuzi wa hali ya hewa.

Jaji kutoka San Francisco hajabainisha wazi kiasi ambacho wamiliki wa magari hayo watalipwa na kampuni ya Volkswagen pale watakapo iuzia kampuni hiyo magari yake wanayoyamiliki.

Makubaliano mengine yaliyofikiwa ni kwamba Volkswagen itatakiwa kutoa fungu la fedha ili kuhamasisha tekinolojia ya kijani.

Wakili anayeiwakilisha kampuni ya Volkswagen Robert Giuffra,amesema kampuni hiyo imekuwa ikifanya jitihada zote kuhakikisha inapunguza uchafuzi wa hewa

Upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili David Boies umesema unataraji haki itatendeka kwa wamiliki wa magari hayo.Joyce Ertel Hulbert,ni mmoja wa wamiliki wa magari aina ya Volkswagen yeye anadai anadai kampuni hiyo imemuangusha

Haki miliki ya picha AFP

Katika hatua nyingine maafisa kutoka taasisi ya kuzuia udanganyifu wa kifedha kutoka ufaransa,wamezivamia ofisi za Peugeot citroen ,ikiwa ni muendelezo wa uchunguza dhidi ya uchafuzi wa hewa kutokana na magari.

Msemaji wa kampuni hiyo anasema wameonyesha ushirikiano wa kutosha katika kuchunguzwa kwao .