Profesa auawa na wapiganaji Bangladesh

Image caption Picha ya Profesa Rezaul Siddique

Profesa mmoja wa Bangladesh ameuliwa na mtu anayeshukiwa kuwa mpiganaji wa Kislamu.

Polisi katika mji wa Rajshahi, kaskazini magharibi mwa nchi, wanasema Rezaul Karim Siddique, ambaye alikuwa profesa wa Kiingereza, alishambuliwa kwa mapanga, wakati akisubiri basi.

Jamaa zake wanasema, alikuwa mhariri wa gazeti kuhusu vitabu, na alianzisha shule ya muziki.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwili wa Professa Rezaul

Kumetokea mauaji kadha nchini Bangladesh katika miezi ya karibuni, ya watu wasiofuata dini, wanaoandika mtandaoni;

lakini mwenzake Professor Siddique, anasema msomi huyo hakupata kuandika au kuzungumza hadharani dhidi ya dini.