Rais asema atapigania Brazil iondolewe kwenye muungano

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dilma Rousseff

Rais wa Brazil Dilma Rousseff amasema kuwa ataomba muungano wa nchi za Marekani ya Kusini kuifukuza Brazil wakati anapokabiliwa na mpango wa kumuondoa madarakani.

Bi Rousseff mara nyingi ameutaja mpango huo kama mapinduzi ya kisiasa yanayofanywa na maadui zake kwa lengo la kumuondoa madarakani.

Amelaumiwa kwa kuilainisha bajeti kabla ya uchaguzi wa mwaka 2014 lakini yeye amekana kufanya lolote baya.

Muungano wa nchi za Marekani Kusini una kipengee kinachoweza kutumiwa ikiwa serikali iliuochaguliwa itapinduliwa.

Ikiwa hatua hiyo itaidhinishwa basi vikwazo kadha vinaweza kuwekewa nchi husika.