Huduma za Apple zafungwa China

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Huduma za Apple zafungwa China

China imezifunga huduma za kampuni ya Apple katika mtandao pamoja na zile za filamu,katika harakati ya kuweka sheria kali zitakazosimamia kile kitakachochapishwa mtandaoni.

Sheria zilizotolewa mnamo mwezi Machi mwaka jana zinakataza umiliki wa kigeni katika huduma za uchapishaji katika mitandao.

Sheria hizo pia zinahitaji kwamba kile kitakachowekwa katika mitandao au kurushwa hewani kama filamu kwa manufaa ya raia wa China kupitia huduma za China.

Apple imesema kuwa ina matumaini kwamba huduma hizo zitarejeshwa hivi karibuni.