Mwanafunzi wa Sudan Kusini kizuizini Canada

Haki miliki ya picha Government of Canada George FG Stanle
Image caption Canada

Wakuu wa Canada wanasema wamemuweka kizuizini mwanafunzi wa shule ya sekondari kutoka Sudan Kusini, kwa sababu wanaamini ana umri wa miaka 29 na siyo 16, kama aliyvodai alipoingia nchini.

Jonathan Nicola anasemekana alikuwa mchezaji mzuri wa mpira wa kikapu, katika timu ya shule yake ilioko Windsor, Ontario.

Maafisa wa mpakani, wanasema mwaka jana, paspoti ya Jonathan Nicola, ilionesha kuwa alizaliwa 1998, lakini ombi lake la visa ya kuingia Marekani, lilionesha chapa yake ya kidole, ilifanana na mtu aliyezaliwa 1986.

Sasa anaweza kufukuzwa nchini.