Jaji mkuu India nusura alie machozi hadharani

Haki miliki ya picha PTI
Image caption Jaji Thakur alimuomba Waziri Mkuu Modi alete mabadiliko

Jaji mkuu wa India, ametoa ombi kwa hamasa, kutaka nchi iajiri majaji zaidi.

Katika hotuba iliyotolewa mbele ya waziri mkuu, Narendra Modi, jaji mkuu, T.S. Thakur, alionekana karibu kulia,machozi yakimlenglenga alipouliza vipi majaji elfu ishirini na moja 21,000 wa India, wanamudu kusikiliza kesi 300-milioni zinazosubiri kufikishwa mahakamani.

Jaji Thakur alimuomba Waziri Mkuu Modi alete mabadiliko kwa kufikiria walioanzisha mashtaka, watu wanaosubiri magerezani, na maendeleo ya nchi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jaji mkuu wa India, ametoa ombi kwa hamasa, kutaka nchi iajiri majaji zaidi.

Bwana Modi amesema serikali itajaribu kutafuta ufumbuzi.

Waziri Modi aliahidi kutekeleza mabadiliko kamilifu katika wizara ya haki.