Al-Shabab aliyejiunga na IS anaswa Somalia

Shabab Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hassan Mohamed alijiondoa al-Shabab mwishoni mwa 2015

Kamanda wa kundi la al-Shabaab aliyejiunga na kundi linalojiita Islamic State nchini Somalia amekamatwa na maafisa wa usalama nchini humo.

Hassan Mohamed Siad ambaye pia hujulikana kama Hassan Fanah alikamatwa Jumapili baada ya maafisa wa ujasusi wa Somalia kufanya operesheni katika nyumba moja mtaa wa Kahda.

Vyombo ya habari nchini Somalia vinasema alikuwa anajificha katika mtaa huo kutoka wa wapiganaji wa al-Shabab.

Serikali ya Somalia ilikuwa imeahidi zawadi ya $2,000 kwa mtu ambaye angetoa habari za kusaidia kukamatwa kwake.

Kamanda huyo alijiunga na kundi la Islamic State mwishoni mwa mwaka 2015.

Serikali ya Somalia inamtuhumu kwa kuhusika katika mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Somalia na vikosi vya Umoja wa Afrika (Amisom) mjini Mogadishu.