ANC yamtuhumu Malema kwa uhaini

Image caption ANC yamtuhumu Malema kwa uhaini

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimemtuhumu kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF),Julius Malema kwa uhaini.

Kiongozi huyo wa EFF anadaiwa kusema ''kuwa serikali ya rais Jacob Zuma inapaswa kukoma kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wanaoandamana kwa amani la sivyo itang'olewa madarakani kwa mtutu wa bunduki.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Msemaji wa ANC Zizi Kodwa anasema matamshi ya Malema ni tishio kwa usalama wa taifa

''Matamshi hayo ni ya kutishia amani na utangamano nchini Afrika Kusini kwa hakika hayo ni matamshi ya uhaini na hatua kali zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya Malema'' msemaji wa ANC Zizi Kodwa alisema.

''Tunaiomba serikali ichukue hatua kali zaidi dhidi ya matamshi hayo ilikuzuia visa vya utovu wa usalama''

Katika mahojiano ya moja kwa moja na shirika la habari la Al Jazeera, bw Malema, alisema kuwa matokeo ya uchaguzi wa 2014 katika jimbo la Gauteng hayakuwa ya haki na akaonya dhidi ya wizi wa kura katika uchaguzi ujao wa kimkoa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uchaguzi huo wa mashinani unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti.

Uchaguzi huo wa mashinani unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti.

''Sehemu moja ya wajibu wetu wa mapinduzi ni kupigana na iwapo itatubidi ,hatutakuwa na ila bali kuchukua silaha na kutetea haki zetu.Tutapigana. alisema bw Malema.

Chama tawala cha ANC kinamtuhumu Malema kwa kukiuka kanuni za kitaifa za uchaguzi kwa kuwachochea watu wapigane.

Kodwa alisema kuwa hiyo ni kinyume cha sheria ya nchi.