Jenerali wa jeshi na mkewe wauawa Burundi

Kararuza Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jenerali Athanase Kararuza wakati mmoja alihudumu kama kamanda wa vikosi vya AU nchini CAR

Afisa mkuu wa jeshi la Burundi ameuawa pamoja na mkewe baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura.

Jenerali Athanase Kararuza na mkewe wameuawa wakiwapeleka watoto wao shuleni, afisa mmoja wa usalama ambaye hakutaka jina lake litajwe ameambia shirika la habari la AFP.

Wizara ya ulinzi imethibitisha kifo chake.

Jenerali huyo ndiye afisa wa karibuni zaidi wa jeshi kuuawa katika mji huo mkuu wa Burundi tangu kufanyika kwa jaribio la kupindua serikali ya Rais Pierre Nkurunziza mwaka jana.